Upcoming Rides &
Competitions
Matukio yote ya baiskeli Tanzania yapo hapa—status, slots, location, na kila kitu unachohitaji kujua.
Hili ni shindano la siku moja litakalowakutanisha wapenda baiskeli kutoka maeneo mbalimbali. Shindano hili litaambatana na sherehe kubwa ya uzinduzi wa Cross Tanzania Cycling Sports Promotion pamoja na Lake Zone Cycling Tour. Sherehe hiyo itafanyika katika viwanja vya CCM Kirumba, Mwanza. Mshindi wa kwanza atajishindia zawadi ya TSh Milioni 1 pamoja na baiskeli. Kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo: Ngoma za asili Wasanii mbalimbali Mashindano ya baiskeli kwa walemavu Mkesha maalum wenye vinywaji na nyama choma
Hili ni shindano la kimataifa litakaloshirikisha timu mbalimbali kutoka Afrika na nje ya Afrika. Mashindano yatazunguka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kukuza michezo, utalii na mshikamano wa jamii kupitia mchezo wa baiskeli. Timu na washiriki wote wanakaribishwa kushiriki katika tukio hili kubwa la kihistoria.